ELIMU YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YAWAFIKIA WALIMU ZANZIBAR
Awareness 24 October 2026 3 min read

ELIMU YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YAWAFIKIA WALIMU ZANZIBAR

Walimu wa Chuo cha Kiislamu Mazizini Zanzibar, tarehe 24 Oktoba, 2026 wamepatiwa mafunzo ya dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi yaliyoandaliwa na PDPC.
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha walimu hao kujua haki na wajibu wao kama wahusika wa taarifa na pia kama wakusanyaji na wachakataji wa taarifa binafsi hasa kwa wakati huu wa ukuaji wa sayansi na teknolojia ambapo jamii inapaswa kulinda taarifa binafsi wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Mafunzo hayo ya siku moja yametolewa na watumishi wa PDPC ikiwa ni njia ya kuhakikisha utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi unazingatiwa.