Watumishi na wataalamu kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) wakiwa tayari kwenye viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela jijini Dodoma kwaajili ya kushiriki maonesho ya wakulima (nane nane) - 2026, kanda ya Kati.
Kupitia maonesho haya, PDPC imejipanga vema kutoa elimu kwa umma kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, taasisi za Umma na Binafsi namna ya kujisajili kwenye Mfumo wa Usajili na Malalamiko wa PDPC, namna ya kujaza na kuwasilisha malalamiko ya uvunjifu wa faragha kupitia mfumo wa Usajili na Malalamiko wa PDPC na namna ya kuomba kibali cha kusafirisha Taarifa Binafsi nje ya mipaka ya Tanzania.
Maonesho haya ya siku nane (8) yaliyobebwa na kaulimbiu ya Tambua Soko, Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050 yanafunguliwa rasmi leo Agosti 01, 2026 na Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
๐๐๐ซ๐ข๐๐ฎ ๐ญ๐ฎ๐ค๐ฎ๐ก๐ฎ๐๐ฎ๐ฆ๐ข๐.