𝐏𝐃𝐏𝐂 𝐍𝐀 π€πˆπ‘π“π„π‹ π“π€ππ™π€ππˆπ€ πŠπ”πˆπŒπ€π‘πˆπ’π‡π€ π”π’π‡πˆπ‘πˆπŠπˆπ€ππŽ πŠπ€π“πˆπŠπ€ π”π‹πˆππ™πˆ 𝐖𝐀 π“π€π€π‘πˆπ…π€ ππˆππ€π…π’πˆ
Event 10 November 2026 3 min read

𝐏𝐃𝐏𝐂 𝐍𝐀 π€πˆπ‘π“π„π‹ π“π€ππ™π€ππˆπ€ πŠπ”πˆπŒπ€π‘πˆπ’π‡π€ π”π’π‡πˆπ‘πˆπŠπˆπ€ππŽ πŠπ€π“πˆπŠπ€ π”π‹πˆππ™πˆ 𝐖𝐀 π“π€π€π‘πˆπ…π€ ππˆππ€π…π’πˆ

Leo Jumanne, Novemba 10, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Dkt. Emmanuel Mkilia alipata amekutana na Bw. Charles Kamoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, ambaye alifika Ofisi za Tume kwa mazungumzo maalum.

Viongozi hao kwa pamoja walizungumza kuhusu namna ya kuboresha ulinzi wa taarifa binafsi na kuelekea kwenye ushirikiano endelevu kati ya PDPC na Airtel Tanzania.

Bw. Kamoto aliweka wazi kuwa, Airtel Tanzania inachukulia ulinzi wa taarifa binafsi kwa uzito mkubwa, si kwa sababu tu ni matakwa ya kisheria, bali kwa kuwa ni jukumu la msingi na sehemu ya shughuli zao za kila siku.

Dkt. Mkilia alitoa pongezi kwa Airtel Tanzania akieleza kwamba ushirikiano kama huu una faida nyingi zikiwemo kusaidia kulinda haki ya faragha na taarifa binafsi za watanzania, kuongeza uaminifu katika huduma za kidijitali na kutoa mchango muhimu kwenye utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.