𝐏𝐃𝐏𝐂 π˜π€π’π‡πˆπ‘πˆπŠπˆ πŒπŠπ”π“π€ππŽ 𝐖𝐀 πŠπˆπŒπ€π“π€πˆπ…π€ 𝐖𝐀 π€πŠπˆπ‹πˆ 𝐔𝐍𝐃𝐄 𝐍𝐀 π“π„πŠππŽπ‹πŽπ‰πˆπ€ 𝐙𝐀 πŠπˆπƒπˆπ‰πˆπ“π€π‹πˆ
Event 20 October 2026 3 min read

𝐏𝐃𝐏𝐂 π˜π€π’π‡πˆπ‘πˆπŠπˆ πŒπŠπ”π“π€ππŽ 𝐖𝐀 πŠπˆπŒπ€π“π€πˆπ…π€ 𝐖𝐀 π€πŠπˆπ‹πˆ 𝐔𝐍𝐃𝐄 𝐍𝐀 π“π„πŠππŽπ‹πŽπ‰πˆπ€ 𝐙𝐀 πŠπˆπƒπˆπ‰πˆπ“π€π‹πˆ

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia ameungana na Timu ya Viongozi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiongozwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb.) kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Akili Unde na Teknolojia za Kidijitali (Global AI & Digital Summit 2026) unaofanyika Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 19 hadi 22 Oktoba 2026.
Mkutano huo umeandaliwa na Kundi la Benki ya Dunia (World Bank Group) kwa kushirikiana na Wizara ya Uchumi na Fedha pamoja na Wizara ya Sayansi na TEHAMA za Jamhuri ya Korea kwa lengo la kujadili matumizi yenye maadili ya Akili Unde katika sekta za kilimo, afya, elimu, utalii na huduma za Serikali.
Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unalenga pia kuvutia uwekezaji katika mradi wa Nala Techno Valley, unaopangwa kujengwa Nala jijini Dodoma, katika eneo la ekari 400 zilizotengwa na Serikali ambao utakuwa na vituo mbalimbali kikiwemo kituo cha Taarifa za Akili Unde (AI Data Centr) ili kutoa fursa za ubunifu, ujasiriamali na ajira kwa vijana kupitia teknolojia za kisasa, ikiwemo Akili Unde.
Kwa upande wa PDPC, mkutano huo ni fursa muhimu ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu maendeleo ya teknolojia za Akili Unde na umuhimu wa kuhakikisha matumizi yake yanazingatia ulinzi wa taarifa binafsi, haki ya faragha na maadili ili wananchi wanufaike na maendeleo salama ya kidijitali.