BODI YA PDPC YAPITIA UTENDAJI KAZI WA TUME KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027
Event 13 November 2026 3 min read

BODI YA PDPC YAPITIA UTENDAJI KAZI WA TUME KWA ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2026/2027

Leo, Novemba 13, 2026. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Mhe. Balozi Adadi Rajabu, ameongoza Kikao cha Kumi na Moja cha Bodi hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Tume kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2026.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi ya PDPC jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya usimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Tume, sambamba na kufuatilia maendeleo ya shughuli zake katika kuhakikisha ulinzi wa taarifa binafsi unaimarishwa nchini.