π–π€πŠπ€π™πˆ 𝐖𝐀 πƒπŽπƒπŽπŒπ€ π–π€πŠπŽπ’π‡π–π€ 𝐍𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐂, πŒπ€πŽππ„π’π‡πŽ π˜π€ π–πˆπŠπˆ π˜π€ π”π“π”πŒπˆπ’π‡πˆ 𝐖𝐀 π”πŒπŒπ€ - πŸπŸŽπŸπŸ”
Event 20 June 2026 3 min read

π–π€πŠπ€π™πˆ 𝐖𝐀 πƒπŽπƒπŽπŒπ€ π–π€πŠπŽπ’π‡π–π€ 𝐍𝐀 𝐏𝐃𝐏𝐂, πŒπ€πŽππ„π’π‡πŽ π˜π€ π–πˆπŠπˆ π˜π€ π”π“π”πŒπˆπ’π‡πˆ 𝐖𝐀 π”πŒπŒπ€ - πŸπŸŽπŸπŸ”

Wakazi mbalimbali wa Jiji la Dodoma wametembelea banda la Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) na kujifunza kazi na majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na PDPC kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2026 yanayoendelea jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la PDPC na kupatiwa elimu kuhusuΒ Tume inavyotekeleza majukumu yake, Bw. Victor John, amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa na PDPC na jinsi huduma hizo zinavyokuwa msaada kwa wananchi.

β€œKwa kweli, hii Taasisi imekuja wakati muafaka wa kidigitali na nimeridhishwa na PDPC kwa huduma nzuri wanayotoa katika maonesho haya kwani nimepokelewa vizuri na kujifunza mengi kuhusu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Pia, huduma za kusajili taasisi zinazokusanya na kuchakata Taarifa na kupata vyeti kwa urahisi kupitia mfumo,” amesema Bw. John.

Aidha Bw. John alitoa ushauri kwa Tume kuweka nguvu kubwa kwenye Elimu kwa Umma na kuongeza ofisi kwaajili ya kutoa huduma kwenye mikoa.

β€œNashauri hii Tume iweke nguvu kwenye kujitangaza kwakua ni mpya watu wengi hawaifahamu hivyo itakua vema ikiweka nguvu kwenye kuelimisha watanzania kuhusu uwepo wa Tume hii na ikiwezekana wafungue matawi kila mkoa” alisema Bw. John

Katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma, wananchi wanapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali yahusuyo PDPC ikiwemo Majukumu ya Tume na namna ya kuutumia mfumo wa Usajili na Malamiko.