BODI YA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI

Bodi ya PDPC

Uongozi

Wajumbe wa Bodi

Balozi Adadi Mohamed Rajabu

MWENYEKITI

Bi. Fatma Mohammed Ali

MAKAMU MWENYEKITI

Bw. Ramadhani Athuman Mungi

MJUMBE

Bw. Hamid Haji Machano

MJUMBE

Bw. Edward Samwel Lyimo

MJUMBE

Bi. Frida Peter Mwera

MJUMBE

Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo ni chombo cha usimamizi wa Tume na kina wajumbe saba ambao ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine watano.

Bodi itasimamia utendaji wa Tume ili kuhakikisha kuwa utendaji huo unazingatia sheria na taratibu zinazosimamia Tume.

Majukumu ya Bodi

1.Kutoa miongozo ya kimkakati na kuunda sera za uendeshaji na usimamizi wa Tume;

2.Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa menejimenti ya Tume;

3.Kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali, ikijumuisha kuidhinishwa kwa mpango kazi wa mwaka, bajeti ya mwaka na bajeti ya nyongeza;

4.Kuidhinisha mipango ya uwekezaji ya Tume;

5.Kuidhinisha ripoti za utendaji kazi wa Tume;

6.Kuidhinisha kanuni za maadili kwa watumishi wa Tume;

7.Kuidhinisha na kusimamia taratibu za usimamizi wa fedha na kanuni za utumishi wa Tume;

8.Kuidhinisha uondoshaji wa mali za Tume; na

9.Kutekeleza wajibu mwingine wowote kwa kadriTume itakavyoona inafaa kwa ajili ya kutimiza malengo yake kwa mujibu wa Sheria hii.