Majukumu ya PDPC yanatokana na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kikijumuisha yafuatayo:
(a) Kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa wakusanyaji na wachakataji;
(b) Kusajili wakusanyaji na wachakataji kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi;
(c) Kupokea, kuchunguza na kushughulikia malalamiko kuhusu madai ya ukiukwaji wa ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu;
(d) Kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya jambo lolote ambalo Tume itaona linaathiri ulinzi wa taarifa binafsi na faragha za watu;
(e) Kutoa elimu kwa umma kwa kadri itakavyofaa kwa madhumuni ya utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi;
(f) Kufanya tafiti na kufuatilia maendeleo ya teknolojia kuhusiana na uchakataji wa taarifa;
(g) Kuanzisha utaratibu wa ushirikiano na mamlaka za nchi nyingine zinazosimamia ulinzi wa taarifa binafsi na kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi; na
(h) Kutekeleza majukumu mengine ya Tume kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.