Uchakataji maana yake ni uchambuzi wa taarifa binafsi, kwa njia za kiotomatiki au vinginevyo, kama vile kukusanya, kurekodi au kushikilia taarifa binafsi au kufanya uchambuzi kwenye taarifa binafsi, ikiwa ni pamoja na-
(a) Kuzipanga upya, kuzichukua na kuzitumia kama zilivyo au kuzibadilisha;
(b) Kuzirejesha au kuzitumia; au
(c) Kuziwianisha, kuzichanganya, kuzuia matumizi yake, kuzifuta au kuziharibu.