Taarifa binafsi maana yake ni taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote, ikiwa ni pamoja na-
(a) Taarifa binafsi zinazohusu rangi, asili ya kitaifa, kikabila, dini, umri au hali ya ndoa ya mtu;
(b) Taarifa binafsi zinazohusu elimu, historia, matibabu, jinai au ajira;
(c) Namba yoyote ya utambulisho, alama au nyingine maalum inayomtambulisha mtu;
(d) Anwani, alama za vidole au kundi la damu binafsi;
(e) Jina la mtu binafsi linaloonekana katika binafsi za mtu mwingine anayehusiana naye
ambapo ufichuzi wa jina hilo utadhihirisha taarifa binafsi za mtu;
(f) Taarifa iliyotumwa kwa mkusanyaji binafsi na mtu, ambayo ni wazi kuwa ni binafsi au ya siri, na majibu kwa taarifa hiyo yanaweza kufichua maudhui ya taarifa ya mtazamo au maoni ya mtu mwingine kuhusu mhusika wa taarifa.