TAARIFA BINAFSI NYETI

Taarifa Binafsi Nyeti

Taarifa binafsi nyeti inajumuisha-

(a) Taarifa ya vinasaba, taarifa inayohusu watoto, inayohusu makosa, miamala ya kifedha binafsi au hatua za kiusalama, taarifa za kibayometriki;

(b) Ikiwa imechakatwa, ni taarifa binafsi inayoonyesha asili ya rangi au kabila, itikadi za kisiasa, imani za kidini au kifalsafa, ushirika, uanachama wa vyama vya wafanyakazi, jinsia na taarifa za kiafya au mahusiano ya kingono; na

(c) Taarifa binafsi yoyote ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi inachukuliwa kuwa ina athari kubwa kwa haki na maslahi ya mhusika wa taarifa