KANUNI ZA MAADILI

Kanuni za Maadili

Kanuni za maadili maana yake ni kanuni zinazobainisha maadili na miiko ya wachakataji na wakusanyaji wa taarifa binafsi zinazoandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 65 cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kinachoelekeza yafuatayo:-

1.Kila mkusanyaji atapaswa kutengeneza kanuni za maadili au sera kwa ajili ya ulinzi wa taarifa binafsi zitakazobainisha maadili na miiko inayopaswa kuzingatiwa wakati wa ukusanyaji au uchakataji wa taarifa binafsi.

2.Kanuni au sera chini ya kifungu kidogo cha (1) zitawasilishwa kwa Tume kwa ajili ya mapitio na kuidhinishwa.

3.Wakati wa mapitio wa kanuni au sera za maadili, Tume itajiridhisha, pamoja na mambo mengine, endapo rasimu za kanuni au sera za maadili zilizowasilishwa zimezingatia masharti ya Sheria hii na ya sekta husika na pale itakapoona inafaa, inaweza kutafuta maoni ya wahusika wa taarifa au wawakilishi wao na kushauriana na mkusanyaji husika kwa madhumuni ya kufanya marekebisho muhimu kabla ya kuziidhinisha.