Huduma

USAJILI

Mtu hatakusanya au kuchakata taarifa binafsi bila kusajiliwa na Tume kama mkusanyaji au mchakataji.

Mchakato wa usajili unafanywa kupitia tovuti ya PDPC www.pdpc.go.tz
Kwa taasisi za umma, zinatakiwa kuwa na nyaraka moja, ambayo ni cheti cha utambulisho wa mlipa kodi cha taasisi 'TIN certificate' ambacho kitatumika kama kiambatisho kwenye fomu ya usajili.
Kwa taasisi binafsi, zinatakiwa kuwa na nyaraka tatu, ambazo ni cheti cha BRELA, cheti cha utambulisho wa mlipa kodi 'TIN certificate' na taarifa ya ukaguzi wa fedha ya mwaka ambazo zitatumika kama viambatisho kwenye fomu ya usajili.
Kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), yanatakiwa kuwa na nyaraka mbili, ambazo ni cheti cha usajili wa NGO na cheti cha utambulisho wa mlipa kodi 'TIN certificate' ambazo zitatumika kama viambatisho kwenye fomu ya usajili.

Kukamilisha usajili tafadhali fuata hatua hizi:

  1. Chagua mtu mmoja kutoka kwenye taasisi/kampuni yako ambaye atasajili taasisi/kampuni kwenye mfumo wa PDPC kwa niaba ya taasisi/kampuni yako. Mtu huyu anajulikana kisheria kama Afisa wa Ulinzi wa taarifa (DPO) na ni lazima kiongozi wa ofisi yako amwandikie barua Mkurugenzi Mkuu wa PDPC kumtambulisha DPO. Barua hiyo ya DPO itawasilishwa PDPC kwa kuiweka kwenye mfumo DPO anapojaza fomu ya usajili.
  2. DPO aingie kwenye tovuti ya PDPC ambayo ni www.pdpc.go.tz
  3. Chagua sehemu iliyoandikwa Usajili
  4. Chagua eneo lililoandikwa ‘Register your organization'
  5. Jaza taarifa za taasisi yako ili kufungua akaunti ya taasisi
  6. DPO atapokea link ya uhakiki itakayotumwa kwenye barua pepe iliyotumika kutengeneza akaunti ya kampuni. DPO anatakiwa kubonyeza link hiyo na itamrudisha sehemu ya kusajili ambapo atatakiwa kuingiza barua pepe aliyotumia kufungua akaunti ya kampuni na neno la siri alilotengeneza kisha atabonyeza neno ‘login’ kuingia na kumaliza kujaza fomu ya usajili.