Huduma

MAFUNZO NA ELIMU KWA UMMA

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imepewa jukumu la kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala yanayohusu ukusanyaji, matumizi, uhifadhi na ulinzi wa taarifa binafsi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imepewa jukumu la kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala yanayohusu ukusanyaji, matumizi, uhifadhi na ulinzi wa taarifa binafsi.
Katika kutekeleza jukumu hili, Tume inalenga kuongeza uelewa wa wananchi, taasisi za umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuhusu haki na wajibu unaohusiana na Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Elimu hii inalenga kuhakikisha kuwa kila mhusika anatambua umuhimu wa kulinda Faragha na usalama wa Taarifa Binafsi katika mazingira ya kidijitali na yasiyo ya kidijitali.
Tume hutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali zikiwemo:
  1. Kampeni za uelimishaji kupitia vyombo vya habari;
  2. Mafunzo, warsha na semina kwa wadau mbalimbali;
  3. Machapisho, miongozo na nyaraka za kielimu;
  4. Matumizi ya majukwaa ya kidijitali ikiwemo tovuti na mitandao ya kijamii.
Kupitia juhudi hizi, Tume inalenga kujenga jamii yenye uelewa mpana wa masuala ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kuongeza uwajibikaji kwa wadau wote wanaoshughulikia Taarifa hizo, na kukuza utamaduni wa kuheshimu Faragha za watu Binafsi.
Aidha, elimu kwa umma ni nyenzo muhimu katika kuzuia ukiukwaji wa Sheria, kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi mabaya ya taarifa binafsi, na kuimarisha imani ya wananchi katika mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa Taarifa.
Tume itaendelea kubuni na kutekeleza mikakati madhubuti ya utoaji elimu kwa umma ili kuhakikisha kuwa kila mdau anakuwa sehemu ya kulinda Taarifa Binafsi na kuzingatia matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa taarifa Binafsi, Sura ya 44.