FEEDBACK & FAQs
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA
Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara
Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara
20 questionsWajibu Mkuu wa DPO ni kuhakikisha Taasisi/Kampuni yake inatekeleza matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya Mwaka 2022 kwa ukamilifu.
Katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa usahihi haya ni baadhi ya majukumu yake kisheria kama yalivyoanishwa kwenye Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi:-
(a). Kuhakikisha Uzingatiaji wa Sheria na Kanuni za Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika uchakataji wa Taarifa Binafsi unaofanywa na mkusanyaji au mchakataji wa Taarifa.
(b). Kutoa Taarifa kwa Tume pale panapokuwa na ukiukwaji wa masharti ya Sheria au Kanuni za Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika uchakataji au ukusanyaji wa Taarifa kwenye Taasisi/Kampuni yake.
(c). Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na kuziwasilisha Tume kila robo mwaka.
(d). Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Faragha ya Taasisi/ Kampuni yake.
(e). Kuomba kibali cha kusafirisha Taarifa Binafsi nje ya mipaka ya Tanzania.
(f). Kuhudhuria Mafunzo maalumu ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa yanayotolewa na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC).
(g). Kuwapa elimu ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Wafanyakazi wenzake.
Kupitia kifungu cha Kumi na nne (14) cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini kila Mtu,Taasisi/Ofisi yoyote iwe ya Umma au Binafsi inayojihusisha na Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi au kimoja wapo yaani Ukusanyaji Pekee/ Uchakataji Pekee anapaswa kujisajili PDPC.
Kiufupi ni Taasisi/Kampuni zote nchini zinapaswa kusajiliwa na kupata Vyeti husika kutoka PDPC kwakua hakuna Taasisi/Kampuni inayoweza kufanya majukumu yake bila Kukusanya na Kuchakata Taarifa Binafsi. Mfano wa Taarifa hizo Binafsi ni kama:-
- Majina ya watu.
- Namba za simu.
- Barua pepe (email).
- Namba ya Kitambulisho. (NIDA, Zanzibar Mkaazi,Leseni)
- Taarifa za afya.
- Taarifa za Kibiometric.
- Taarifa za Wafanyakazi.
- Taarifa za Wateja.
- Taarifa za CCTV.
- Taarifa zozote zinazomtambulisha mtu.
Endapo Taasisi/Kampuni yako inajihusisha na Ukusanyaji, Uchakataji, Uhifadhi au Matumizi Ya Taarifa Binafsi bila kujisajili PDPC, unaweza kukumbana na madhara ya kisheria, kiutendaji na hata kimkakati kwa Ofisi yako.
Haya ndiyo baadhi ya madhara yanayoweza kutokea:
(a). Faini na Adhabu
- Kupewa onyo rasmi na PDPC
- PDPC kukutoza faini, kifungo au vyote kwa pamoja
- Kukosa Huduma mbalimbali za Kiserikali (Mifumo kusomana)
- PDPC Kukuzuia kufanya shughuli za Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi
Hii hutegemea ukubwa wa ukiukwaji na madhara yaliyosababishwa.
(b). Kupoteza Uaminifu wa Wateja
Wateja wanapogundua kuwa taasisi yako:
- haijasajiliwa,
- hailindi Taarifa zao vizuri,
- au haifuati Sheria za Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya Mwaka 2022.
wanaweza kupoteza imani na kampuni yako.
Kumbuka katika Dunia ya kidijitali, Uaminifu wa Wateja ni mtaji mkubwa sana.
(c). Hatari ya Kuvuja kwa Taarifa (Data Breach)
Bila usimamizi wa PDPC:
- Taasisi nyingi hukosa mifumo sahihi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
- Taasisi nyingi hukosa Sera za Faragha au Cybersecurity Controls.
Hii inaweza kusababisha:
- Kuibwa kwa Taarifa Binafsi
- Matumizi mabaya ya Taarifa Binafsi.
(d). Kukosa Fursa za Ushirikiano
Mashirika mengi ya kimataifa, benki, telecoms na Wadau wa maendeleo huangalia Uzingatiaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kabla ya kushirikiana na Taasisi.
Hivyo kutokujisajili kunaweza:
- kuathiri Mashirikiano.
- Zabuni.
- Uwekezaji.
Ndio, kuna malipo. Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya mwaka 2022, Cheti kimoja cha PDPC kinapaswa kuwa kati ya Laki moja ya kitanzania (100,000) mpaka Milioni Moja ya Kitanzania (1,000,000), kwa Vyeti Viwili ni kati ya 200,000/= - 2,000,000/=
NB: Kila Taasisi inapaswa kuwa na Vyeti Viwili yaani Cheti cha kukusanya Taarifa na Cheti cha Kuchakata Taarifa.
Kuna vitu vitatu ambayo vinafanya Gharama ya Vyeti husika kuwa Tofauti na vitu hivyo ni:-
(a) Aina ya Taasisi {Serikali, Binafsi ya Kibiashara au Binafsi ya Kijamii (NG’O)}
(b) Idadi ya Wafanyakazi ( Hii ni kwa Taasisi Binafsi za kibiashara)
(c) Ripoti ya Ukaguzi wa Taarifa za Fedha (Hii ni kwa Taasisi Binafsi za kibiashara)
Endapo Taasisi/Kampuni yako inajihusisha na Ukusanyaji wa Taarifa/ Uchakataji wa Taarifa unahitaji kuwa na vielelezo vifuatavyo ili kufanya na kukamilisha usajili PDPC:-
(a): Barua ya Utambulisho wa Afisa Ulinzi wa Taarifa (DPO) wa Taasisi/Ofisi yako, alieteuliwa na Mkuu wa Taasisi na barua hiyo inapaswa kusainiwa na Mkuu wa Taasisi
(b): Cheti cha Usajili wa Biashara na Leseni.
(c): Ripoti ya Ukaguzi wa Taarifa za Fedha (Financial Statement Audit Report).
N:B Vielelezo namba mbili na tatu ni kwa zile Taasisi/Kampuni za Kibiashara tu.
Usajili unafanyika Mtandaoni (online) kwa asilimia 100, kupitia wavuti yetu ya www.pdpc.go.tz ambapo utaenda moja kwa moja kwenye kitufe kilichoandikwa huduma zetu na utabonyeza sehemu iliyoandikwa Usajili.