FEEDBACK & FAQs
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA
Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara
Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara
20 questionsSiku Tano (5) mpaka Saba (7) za kazi.
Ndio, PDPC wanapokea Malalamiko ya Matumizi Mabaya ya Taarifa Binafsi/ Uvunjifu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya Mwaka 2022.
Unaweza kuwasilisha Malalamiko PDPC kwa njia ya mbili ambazo ni:-
(a). Kwa Njia ya Mtandao, Ingia kwenye tovuti ya PDPC, www.pdpc.go.tz kisha shuka chini bonyeza kitufe kimeandikwa Malamiko baada ya hapo jaza fomu ya malalamiko, (Form No. 1).
NB: Jaza kurasa zote sita ili kukamilisha zoezi la uwasilishaji wa lalamiko.
(b). Kwa Kufika kwenye Ofisi za PDPC, Ofisi ya PDPC - DODOMA inapatikana Jengo la Wizara ya Ujenzi (Mtaa wa Moshi) na Ofisi ya PDPC - ZANZIBAR inapatikana Jengo la Bombay Bazar, Ukifika kwenye moja ya Ofisi zetu utajaza fomu ya malalamiko (Form No.1) na kukamilisha zoezi la uwasilishaji wa lalamiko.
NB: Ni vema ukaja na nakala (copy) ya vielelezo vyote muhimu kulingana na lalamiko lako.
Ndio, unaweza kuwasilsha lalamiko/malalako PDPC endapo muhusika wa Taarifa Binafsi ambae faragha yake imevunjwa ni
- Mtoto (yaanu Umri wake ni chini ya Miaka 18),
- Mgonjwa
- Marehemu.