FEEDBACK & FAQs
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA
Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara
Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara
20 questionsTume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ni Tume huru iliyoanzishwa na serikali ilikusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya mwaka 2022, ambapo malengo ya Sheria hii ni:-
(a) Kudhibiti ukusanyaji na uchakataji wa Taarifa Binafsi.
(b) Kuhakikisha kwamba Ukusanyaji na Uchakataji wa Taarifa Binafsi za Mhusika wa Taarifa unaongozwa na misingi iliyowekwa katika Sheria hii.
(c) Kulinda faragha za watu Binafsi.
(d) Kuweka utaratibu wa kisheria na kitaasisi wa kulinda Taarifa Binafsi.
(e) Kuwapa wahusika wa Taarifa haki na nafuu katika kulinda Taarifa Binafsi kutokana na Ukusanyaji na Uchakataji usiofuata masharti ya Sheria hii.
Tume hii ilianzishwa rasmi tarehe 01 Mei, 2023 kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya Mwaka 2022.
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini.
(b) Kusajili wakusanyaji na wachakataji wa Taarifa Binafsi nchini.
(c) Kupokea, kuchunguza na kushughulikia malalamiko kuhusu madai ya ukiukwaji wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Faragha za watu.
(d) Kufanya tafiti na kufuatilia maendeleo ya Teknolojia kuhusiana na Uchakataji wa Taarifa.
(e) Kuimarisha mashirikiano na nchi zingine.
Ni Taarifa yoyote inayoweza kumtambulisha mtu. Mfano Majina, Barua Pepe, Namba ya Simu, Namba ya Kitambulisho n.k.
Kuna aina mbili za Taarifa Binafsi nazo ni:-
(a)Taarifa Binafsi za kawaida:- Hizi ni Taarifa Binafsi za kawaida zinazoweza kumtambulisha mtu na endapo zikitumika vibaya madhara yake yanaweza yasiwe makubwa sana. Mfano Majina, Namba za Simu, Namba za kitambulisho (Nida, Zanzibar Mkaazi, Leseni, Pasi ya kusafiria) n.k
(b) Taarifa Binafsi Nyeti:- Hizi ni Taarifa Binafsi nyeti zinazoweza kumtumbulisha mtu na endapo Taarifa hizi zikitumika vibaya zinaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika wa Taarifa. Mfano Taarifa za Vinasaba (DNA), Alama za Vidole, Macho, Sura (Biometric) Taarifa za Afya, Taarifa za Kibenki, Taarifa za Dini, Taarifa za Kisiasa, Taarifa za hali ya ndoa, familia na watoto kwa ujumla n.k
Mkusanya Taarifa ni Mtu, Taasisi/Ofisi yoyote iwe ya Umma au Binafsi inayokusanya Taarifa Binafsi kutoka kwa Muhusika wa Taarifa.
Mchakata Taarifa ni Mtu,Taasisi/Ofisi yoyote iwe ya Umma au Binafsi ambayo inachakata (inatumia) Taarifa Binafsi ili kumpatia huduma Mhusika wa Taarifa kwa niaba ya Mkusanyaji wa Taarifa.
DPO ni mtu yeyote aliyeteuliwa na Mkusanyaji/Mchakataji wa Taarifa Binafsi (Mkuu wa Taasisi,Kampuni/Ofisi) na kupewa jukumu la Kusimamia Utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi,Sura ya 44 ya mwaka 2022 (PDPA) kwenye Taasisi/Ofisi yake.
Mtu yoyote anaweza kuwa Afisa Ulinzi wa Taarifa (DPO) wa Taasisi/Kampuni bila kujali Taaluma yake au Uraia wake, kikubwa awe na umri wa kuanzia mika 18 na kuendelea pia awe na akili timamu.